Kivuko cha waenda kwa miguu cha projekta mahiri kimeanza kutumika mjini Huaibei,mkoani Anhui, China. Kifaa hiki ni kifaa cha usalama barabarani cha kisasa cha akili bandia kinachotumia projekta. Mchana huonekana kama kivuko cha kawaida cha waenda kwa miguu; usiku kinajiwasha chenyewe. Taa inapokuwa nyekundu, uso wa barabara huonyesha kwa projekta mistari myekundu ya kivuko na michoro ya katuni ya askari wa usalama barabarani, na kuonyesha maneno ya kukumbusha ni wakati wa taa nyekundu, watu wasivuke, tafadhali subiri; taa inapokuwa ya kijani, hubadilika na kuwa mistari ya kijani ya kivuko, ikionyesha alama ya taa ya kijani na kuwakumbusha watu kuvuka,na hutoa sauti ya tahadhari ya usalama. Projekta inaonekana wazi na kueleweka moja kwa moja, inarahisisha madereva kuona watembeaji miguu kutoka mbali, na kwa kutumia teknolojia inalinda usalama wa usafiri wa wananchi.
