Kongamano la Uchumi wa Buluu la kimataifa kufanyika Dar es salaam Septemba

Kongamano la Tano la Kimataifa la Uchumi wa Buluu linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 7 hadi 9, 2026, likiwa na kaulimbiu “Kuwezesha Shughuli za Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo Endelevu Afrika.”

Mkuu wa Chuo cha Bahari cha Tanzania, Profesa Tumaini Ngurumo, amesema mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amesema kongamano hilo linakuja wakati nchi mbalimbali za Afrika zikizidi kutumia rasilimali za bahari kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi, ajira na kuongeza kipato kwa wananchi.

Kongamano hilo litawakutanisha wadau wa uchumi wa buluu kutoka Tanzania na nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, maarifa na tafiti zinazolenga kuongeza tija katika sekta hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live