Rais Xi Jinping wa China amehudhuria Mkutano wa Kitaifa ya Utoaji wa Tuzo za Sayansi na Teknolojia, Mkutano wa 22 wa Wasomi (Academician) wa Chuo cha Sayansi cha China, na Mkutano wa 18 wa Wasomi (Academician) wa Chuo cha Uhandisi cha China, na Mkutano wa 11 wa Kitaifa wa Wajumbe wa Chama cha Sayansi na Teknolojia cha China iliyofanyika jana Jumatano asubuhi katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing.Akihutubia mikutano hiyo, Rais Xi amesisitiza kuwa, “Mpango wa 15 wa Maendeleo wa Miaka Mitano” ni kipindi muhimu cha China cha kujenga nchi yenye nguvu kubwa ya kisayansi na kiteknolojia, na kwamba ni lazima kuchukua fursa hii ya kihistoria, kuharakisha mchakato wa kujiimarisha katika sayansi na teknolojia yenye kiwango cha juu, kusonga mbele kwa hatua madhubuti na kufikia lengo la kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya kisayansi na kiteknolojia ifikapo mwaka 2035, ili kuunga mkono na kuelekeza ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China kwa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia.
