Rais Xi Jinping wa China na mkewe Bibi Peng Liyuan jana Novemba 18 waliandaa dhifa mjini Shenzhen mkoani Guangdong, kuwakaribisha wageni wanaohudhuria mkutano wa 33 usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC).
Kwenye hotuba yake, Rais Xi aliwakaribisha wageni wote kwa niaba ya serikali ya China na watu wake. Alisema ufunguaji wa mlango umekita mizizi katika mji wa Shenzhen na uvumbuzi unaendesha nguvu ya mji huo, huku ushirikiano ukiwa chanzo cha nguvu yake, akiongeza kuwa mafanikio ya Shenzhen pia ni mfano mdogo wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China, na pia ni mfano wa ushirikiano wenye mafanikio katika Asia-Pasifiki.
Akibainisha kuwa ufunguaji mlango, uvumbuzi na ushirikiano vimekuwa sifa za kipekee za APEC tangu kuanzishwa kwake, Rais Xi alisema APEC imefuata mwelekeo wa nyakati na kuongoza mchakato wa mafungamano ya kiuchumi ya kikanda, na kuifanya Asia-Pasifiki kuwa kanda yenye nguvu zaidi na injini muhimu ya ukuaji wa uchumi wa dunia.