Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres, ameonya dunia imeingia katika eneo hatari la hali mbaya ya hewa, huku athari za El Niño zikianza kuhisiwa duniani kote.
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), limetoa takwimu za hivi karibuni kuhusu hali mbaya zaidi ya hewa kwa zaidi ya miaka 70 ambayo huenda ikaendelea hadi mwezi Februari 2027.
Mamlaka za hali ya hewa pia zimesema, El Niño itaongeza hali ya joto katika baadhi ya maeneo, pamoja na kuongeza kiwango cha juu cha joto linaloongezeka kote duniani kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu.
El Niño hubadilisha mifumo ya hali ya hewa kote ulimwenguni, ikisukuma baadhi ya maeneo kwenye ukame huku mengine yakipata vimbunga vikali na mafuriko.
