Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeonya kwamba mifumo ya usaidizi na ulinzi katika kambi za wakimbizi duniani iko katika hatari ya kuporomoka kutokana na kuendelea kupunguzwa kwa ufadhili.
Hatua hiyo imesababisha karibu wakimbizi milioni 8.3, watu waliokimbia makazi yao, na watu wasio na uraia kukosa usaidizi wa kutosha mwaka huu.
Ripoti iliyotolewa na UNHCR imeonyesha kuwa fedha zilizopatikana zilipungua kwa asilimia 24 kutoka dola bilioni 5.2 hadi dola bilioni 3.9 kati ya mwaka 2024 na mwaka 2025. Ripoti hiyo imesema, idadi ya watu wanaohudumiwa na UNHCR inabaki katika kiwango cha juu kihistoria, kinachotarajiwa kufikia milioni 131.2 ifikapo mwisho wa 2026.
