Shughuli maalum kwa Misri chini ya mpango wa “Export to China” zimefanyika mjini Cairo. Hii ni mara ya kwanza mfululizo wa shughuli za “Export to China” kufanyika katika nchi ya Afrika.
Wawakilishi zaidi ya 170 kutoka serikali za China na Misri, vyama vya biashara, na makampuni walihudhuria shughuli hiyo, na makampuni zaidi ya 10 ya Kichina yameshiriki katika upatanishi wa kibiashara. Makampuni ya China na Misri yamesaini mikataba kadhaa ya biashara kuhusu bidhaa kama vile ngozi, kitani, na pamba, huku thamani ya mikataba ikifikia dola za kimarekani milioni 170.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia katika Wizara ya Uwekezaji na Biashara ya Nje ya Misri Fouad amesema uamuzi wa China wa kutekeleza sera ya ushuru sifuri kwa nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China kuanzia Mei 1 mwaka huu, una umuhimu mkubwa, na kumefungua njia pana kwa bidhaa za Afrika, ikiwa ni pamoja na bidhaa za Misri, kuingia kwenye soko la China.
