
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimeelezea wasiwasi kuhusu kuenea kwa kasi kwa mlipuko wa Ebola kijiografia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huo imezidi 5,500.
Meneja wa shughuli za kukabiliana na Ebola katika Africa CDC Wessam Mankoula akihutubia mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kamati ya Mawaziri ya Afrika katika makao makuu ya Africa CDC huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ameonya kuhusu kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo katika eneo kubwa zaidi la kijiografia katika siku zake 100 za kwanza.
Wakati mlipuko ukiendelea kuenea kote DRC, taarifa mpya kutoka mamlaka ya Africa CDC na DRC zimeonyesha kuwa nchi hiyo ya Afrika ya Kati imerekodi jumla ya wagonjwa 5,514 waliothibitishwa na vifo 2,642, huku kiwango cha vifo kikiwa asilimia 47.9. Jumla ya wagonjwa 1,200 wamepona ugonjwa huo hadi sasa.