
Timu inayosimamia ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 iliwasili Jumatatu wiki hii katika Minembwe, jimbo la Kivu Kusini nchini humo, huku mapigano yakiendelea katika baadhi ya sehemu ya eneo hilo.
Timu hiyo inayojumuisha wataalamu wa kijeshi kutoka kundi la nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) na wawakilishi kutoka serikali ya DRC na kundi la M23, iliwasili kwa helikopita mbili za Ujumbe wa kulinda utulivu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), hatua inayoashiria utekelezaji kivitendo wa mfumo wa uhakiki wa usitishwaji vita kwa mara ya kwanza, siku mbili baada ya serikali ya DRC na kundi la M23 kufikia makubaliano ya kutimiza amani.
Habari zinasema bado kuna mvutano katika jimbo la Kivu Kusini, ambako katika wiki zilizopita, mapigano yaliendelea katika maeneo mengi karibu na Minembwe kati ya kundi la M23 na jeshi la serikali.