Takwimu zilizotolewa jana zimeonesha kuwa, kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimezidi 6,000, huku karibu vifo 3,000 vikihusishwa na ugonjwa huo.
Mamlaka za huko zimeripoti kuwa, mpaka kufikia jumamosi iliyopita, DRC ilirekodi kesi 6,041 zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola katika mikoa sita, ikiwemo vifo 2,911, na kufanya jumla ya kiwango cha vifo kufikia asilimia 48.2, na wagonjwa 1,366 wamepona.
Mlipuko wa Ebola hivi sasa umeathiri maeneo 60 ya afya katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut-Uele, Bas-Uele na Tshopo.
Mlipuko huu wa Ebola uliotangazwa mwezi Mei mwaka huu, umekuwa ni mkubwa zaidi na mbaya zaidi kurekodiwa nchini DRC, na wa pili kwa ukubwa duniani nyuma ya mlipuko uliotokea Afrika Magharibi mwaka 2014 hadi 2016.
