Mkutano wa mifumo ya Chakula Afrika wafunguliwa Rwanda

Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika umefunguliwa katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, na kuleta pamoja watunga sera, wakulima, wawekezaji, watafiti na wenzi wa maendeleo kwa lengo la kujadili njia za kufanyia mageuzi sekta ya chakula na kilimo katika bara la Afrika.

Mkutano huo unajikita katika changamoto kubwa ikiwemo ufadhili, teknolojia, hasara baada ya mvuno, upatikanaji wa soko, na unyumbufu wa mabadiliko ya tabianchi.

Washiriki wamesema Afrika ina fursa kubwa ya kilimo, lakini uwekezaji mdogo na mishtuko inayohusiana na mabadiliko ya tabianchi inaendelea kuwa kikwazo cha uzalishaji na faida, na kuongeza kuwa, mafanikio ya mkutano huo yatategemea kwa kiasi kikubwa katika kubadilisha majadiliano kuwa uwekezaji, uhusiano imara zaidi, upatikanaji wa soko kwa urahisi, na suluhisho la kivitendo kwa wakulima na biashara ya kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live