Kenya yataka kushirikiana na China ili kuboresha viwanda vyake

Kenya inapanga kuimarisha ushirikiano na China ili kuboresha uwezo wake wa uzalishaji viwandani, kuongeza mauzo ya nje ya bidhaa zenye thamani, na kuleta nafasi za ajira kwa vijana.

Maofisa kadhaa wa Kenya walisema hayo jana Alhamisi kwenye Maonyesho ya 9 ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya mjini Nairobi.

Mkurugenzi wa taifa wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Kenya (KNCCI), Joseph Mutavi Kithu, amesema China ni kichocheo cha kimkakati kwa ajili ya ufufuaji wa viwanda nchini Kenya, na kwamba uwezo mkubwa wa China kwenye sekta ya viwanda, uliojengwa kwenye msingi wa teknolojia za kisasa, nguvu kazi yenye ujuzi na minyororo ya usambazaji ya uhakika, unaweza kusaidia maendeleo ya viwanda ya Kenya.

Bw. Kithu ameongeza kuwa Kenya sasa inaleta zana zaidi kutoka China ili iweze kuzalisha bidhaa zaidi nchini Kenya, na pia amewahimiza Wachina kuanzisha biashara Kenya, ili iwe rahisi kwao kulifikia soko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live