Serikali ya Tanzania yapanga kutumia teknolojia kukuza uchumi wa bluu

Serikali ya Tanzania inaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali, mifumo ya kisasa ya usimamizi wa bandari na biashara, pamoja na matumizi ya taarifa za kisayansi katika kufanya maamuzi kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya uchumi wa bluu nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bw.Hamadi Masauni, amesema hayo wakati akihutubia Kongamano la Tano la Kimataifa la Uchumi wa Bluu 2026, lililofanyika Dar es Salaam.

Bw. Masauni amesema uchumi wa bluu wa kisasa unahitaji wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu, ubunifu pamoja na uwezo wa kutumia teknolojia mpya, hivyo taasisi za elimu ya juu na utafiti, ikiwemo Taasisi ya mambo ya bahari (DMI), zina nafasi muhimu katika kuzalisha rasilimali watu wenye uwezo wa kuendesha mabadiliko katika sekta hiyo.

Amesema mafanikio ya uchumi wa bluu yanategemea kwa kiasi kikubwa utafiti wa kisayansi na ubunifu, ambao unalenga kuongeza uelewa kuhusu uwezo wa raslimali zilizopo, kuboresha uzalishaji, kutengeneza bidhaa mpya, kuongeza thamani ya mazao ya bahari na kulinda mazingira.

peartree.co.za

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live