Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Yemen Bw. Hans Grundberg tarehe 7 Septemba alitoa taarifa akisema kundi la Houthi hivi karibuni limefanya mashambulizi katika mistari kadhaa nchini Yemen, kusababisha kuongezeka kwa mapambano ya kisilaha, na kuongeza hatari ya kuzorotesha mgogoro wa nchini humo, hali inayoleta wasiwasi mkubwa.
Taarifa imesema kama Yemen itaangukia tena kwenye mapambano makubwa na endelevu, italeta matokeo mabaya kwa raia wake wa kawaida, na kufanya mchakato mgumu wa utatuzi wa kisiasa uwe na utatanishi zaidi.
Bw. Grundberg ametoa wito kwa pande zote hasimu kusimamisha uhasama mara moja, kujizuia kadri iwezekanavyo, na kutumia kikamilifu njia zilizopo za mawasiliano, ili hali isipambe moto zaidi.
