
Vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) vimeripoti kuwa, wanafunzi 26 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika ajali ya moto mkubwa uliozuka jana huko Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa nchi hiyo.
Ripoti hizo zinasema, miili ya marehemu imepelekwa hospitali za eneo hilo, na idadi kamili ya watu waliofariki bado haijajulikana, na kwamba wanafunzi wengi wanapatiwa matibabu kutokana na kuvuta moshi.
Mashuhuda kadhaa waliwaambia waandishi wa Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, takriban nyumba 80 ziliharibiwa na moto huo.