Baraza Kuu la UM lamruhusu Abbas kushiriki katika mjadala wa jumla kupitia video

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kumruhusu Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kushiriki katika mjadala wa jumla wa mwaka huu kupitia video, kufuatia hatua ya Marekani ya kumnyima viza.

Azimio hilo lililopitishwa kwa kura 152 za ​​ndiyo, 3 za hapana na 4 zisizopigwa, limeamua kuwa Palestina inaweza kuwasilisha taarifa ya Abbas iliyorekodiwa awali, ambayo itaoneshwa katika Ukumbi wa Baraza Kuu wakati wa mjadala wa jumla katika kikao cha 81 baada ya kutambulishwa na mwakilishi wake aliyepo ukumbini.

Azimio hilo pia linaamua kuwa Palestina inaweza kutoa taarifa kupitia mkutano wa video au kuwasilisha taarifa iliyorekodiwa awali katika mikutano ya ngazi ya juu ya kimataifa inayohusu utatuzi wa amani wa suala la Palestina na utekelezaji wa suluhisho la mataifa mawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live