Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco tarehe 29 Septemba alimteua Fatima Ezzahra El Mansouri kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, na kumpa idhini ya kuunda baraza jipya la mawaziri. Bibi El Mansouri amekuwa mwanamke wa kwanza kuwa mkuu wa serikali katika historia ya Morocco.
Bibi El Mansouri ni Mratibu wa Kitaifa wa Chama cha Uhalisia na Usasa cha Morocco(Authenticity and Modernity Party PAM). Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Abdelouafi Laftit tarehe 24 alitangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge nchini humo. Chama cha PAM kilishinda viti 97 kati ya viti 395 vya Baraza la Wawakilishi, na kuongoza katika uchaguzi huo. Kwa mujibu wa katiba ya Morocco, Mfalme anateua mkuu wa serikali kutoka katika chama chenye viti vingi zaidi katika Baraza la Wawakilishi, ambaye atawajibika kuunda serikali mpya.
