China yatoa msaada wa dola milioni 2 kwa Kenya kukabiliana na Ebola na kupunguza ukame

Kenya imepokea msaada wa dola milioni 2 za kimarekani kutoka kwa China ili kusaidia kukabiliana na Ebola na kupunguza athari za ukame.

Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan, Katibu Mkuu wa Hazina Bw. Chris Kiptoo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Umma Bibi Mary Muthoni walihudhuria sherehe ya makabidhiano mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambapo pande hizo mbili zilisaini hati za makabidhiano.

Msaada huo ni mwitikio wa ombi kutoka kwa serikali ya Kenya, dola milioni 1 zitatumika kuimarisha miundombinu ya maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, na nyingine milioni 1 zitatumika kusaidia mwitikio wa serikali ya Kenya kutokana na athari za ukame.

Balozi Guo amesema msaada huo kwa Kenya unaonyesha hisia ya urafiki ya serikali ya China na watu wake kwa serikali na watu wa Jamhuri ya Kenya, na kuongeza kuwa China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa maendeleo na Kenya chini ya mifumo ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Pendekezo la Maendeleo ya Dunia (GDl).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live