
Mkutano wa 52 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ulifungwa jana huko Baghdad, Iraq. Naibu Waziri Mkuu wa Iraq na Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Fuad Hussein amesema mkutano huo umepitisha “Azimio la Baghdad”, na kuwa Iraq inadumisha mawasiliano na Iran na nchi za Ghuba, ikijitahidi kuwezesha mkutano kati ya pande husika huko Baghdad.
Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika baada ya kufungwa kwa mkutano huo, Bw. Hussein amesema suala la Palestina lilipewa kipaumbele kwenye ajenda. Mkutano huo pia ulijadili usalama wa kikanda, hali ya kibinadamu, ushirikiano wa kiuchumi, na usalama wa chakula na maji.
Mkutano huo wa siku mbili ulikuwa na kauli mbiu ya “Mazungumzo na Mshikamano: Nguzo Mbili za Amani na Maendeleo Endelevu.” Waziri Mkuu wa Iraq Bw. Ali al-Zaidi alihudhuria sherehe ya ufunguzi tarehe 17, ambapo Iraq ilichukua rasmi uenyekiti wa zamu wa baraza hilo.