Timu ya uokoaji ya China yagundua ishara za uhai chini ya kifusi cha jengo lililoanguka Nairobi

Timu ya uokoaji ya China imegundua ishara za uhai chini ya kifusi cha jengo lililoanguka mjini Nairobi, Kenya, ikileta matumaini ya kupata manusura wakati operesheni za pamoja za uokoaji zinaendelea.

Maneja wa operesheni za dharura wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na ofisa anayesimamia operesheni za shirika hilo kwenye eneo la tukio, Anthony Muchiri, amesema waokoaji wa Shirika la Blue Sky Rescue (BSR) kutoka China wamegundua ishara mbili tofauti za uhai chini ya kifusi cha jengo lililoporomoka kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Mwokoaji wa BSR, Zhang Yuran amesema timu hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kutafuta ishara za uhai na kushirikiana na timu nyingine za ukoaji kwenye eneo la tukio.

Amesema waokoaji wameanza kufungua njia za kufikia sehemu mbili ambapo ishara za uhai zilipatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live