UM wahamasisha raslimali za ziada kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya kibinadamu kaskazini Ethiopia  

Mahitaji ya kibinadamu yameongezeka kutokana na uhasama unaoendelea kaskazini mwa Ethiopia, na kufanya mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kuhitaji kuhamasisha raslimali za ziada, ikiwa ni pamoja na kurekebisha hatua ya kutoa ufadhili.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuongeza kukusanya ufadhili wa ziada wa haraka ili kuendelea kuongeza msaada kwa ajili ya watu wanaohitaji katika maeneo ya Afar, Amhara na Tigray.

Wakati huo huo, mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Ethiopia Bw. Ozonnia Ojielo anaendelea kushirikiana na mamlaka ya kikanda ili kuhakikisha upatikanaji salama wa kibinadamu na usafirishaji wa msaada wa kuokoa maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live