IOM: Waethiopia 50,000 wakimbilia Kenya kufuatia mapigano

Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) limesema kuwa takriban Waethiopia 50,000 wamekimbilia nchi jirani ya Kenya kutafuta usalama, kufuatia mapigano makali kusini mwa Ethiopia.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wahamiaji limeonya kuwa kuwasili kwa watu zaidi kunaweza kuongeza shinikizo kwenye huduma na rasilimali za wenyeji, ambazo tayari zimelemewa.

Takwimu za IOM zinaonyesha kuwa kufikia Alhamisi, takriban watu 50,000 wamefika Moyale, kaunti ya Marsabit na wanaishi na jamii za wenyeji kando ya mpaka au wanahifadhiwa katika maeneo matano ya muda.

Kutokana na hali inavyoendelea kubadilika, IOM imesema kuwa serikali ya Kenya na mashirika washirika wanajiandaa kutoa msaada kwa hadi watu elfu 80, wakitarajia kuwa watu wengine zaidi watawasili na kwamba mahitaji ya kibinadamu yataongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live