
Waziri wa muda wa habari na huduma za mawasiliano wa Jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini William Wol Mayom Bol amesema idadi ya vifo vinavyotokana na ghasia mpya za kikabila katika Kaunti ya Tonj Kaskazini imeongezeka hadi 84.
Bol alisema watu 12 zaidi waliuawa na wengine 13 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi dhidi ya kijiji cha Bundir huko Akop Payam Jumanne. Pia alielezea kuwa shambulizi hilo ni kama “limefanywa bila sababu” na “lililoratibiwa.”
Shambulizi hilo jipya la kikatili lilifuatia shambulizi la Jumatatu lililofanywa na vijana wenye silaha kutoka Kaunti jirani ya Mayom katika Jimbo la Unity, ambalo lilisababisha vifo vya watu 72. Sudan Kusini hivi karibuni imeshuhudia kuongezeka kwa ghasia za kikabila kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba.