Mkutano wa APEC wa Shenzhen ni kilele kipya katika ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kuwa Mkutano wa 33 usio rasmi wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) umefikia kilele kipya katika ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki. Bw. Wang amesema hayo katika mkutano na wanahabari uliofanyika baada ya mkutano huo mjini Shenzhen, mkoani Guangdong kusini mwa China. Ameongeza kuwa mkutano huo umekuwa tukio muhimu zaidi la kidiplomasia lililoandaliwa na China mwaka huu. Ameeleza kuwa mkutano huo ulizaa “Dira ya Viongozi wa APEC ya Shenzhen” yenye malengo makubwa, inayotekelezeka na ya kina, ambayo ni matokeo muhimu zaidi ya “Mwaka wa China” wa APEC na hatua muhimu mpya katika ushirikiano wa APEC.

Katika mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China alitoa wito wa kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye sifa za mshikamano na kusaidiana, uwazi na mafungamano, ujasiriamali na uvumbuzi, pamoja na maendeleo jumuishi. Bw. Wang amebainisha kuwa Rais Xi amefafanua mapendekezo ya China kuhusu aina ya jumuiya ya Asia-Pasifiki inayopaswa kujengwa na jinsi gani ya kuijenga.

Akizungumzia kuhusu mkutano wa kilele kati ya China, Russia, na Marekani, ambao ameuita ni tukio la kihistoria litakalokumbukwa daima, Bw. Wang amesema mkutano huo ulikuwa wa kwanza kabisa wa ana kwa ana kati ya wakuu wa nchi hizo tatu, na una umuhimu mkubwa wenye athari za mbali.

Mkutano huo kati ya Rais wa China Xi Jinping, na wenzake wa Russia Vladimir Putin, na Marekani Donald Trump ulifikia makubaliano muhimu. Azimio la nchi za China, Russia, na Marekani kuhusu Amani lililotolewa baada ya mkutano huo ni nyenzo muhimu katika kushughulikia changamoto za kimataifa na kudumisha amani na utulivu duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live