Hafla ya mawasiliano ya kiutamaduni yenye kaulimbiu “Kujionea Ustaarabu wa China: Kurithi Historia, Kushirikiana Kuunda Mustakabali” ilifanyika Septemba 23 mjini Beijing. Ujumbe wa walimu na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Millburn ya Ireland ya Kaskazini, Uingereza, ulitembelea Shule ya Wangfu yaBeijing ili kushiriki katika mazungumzo ya ana kwa ana na wenzao wa China na kujionea kwa karibu utamaduni wa China.
