Watu wengi wanajiburudisha katika eneo la kupumzika lenye baridi huko Sipailou mjini Hangzhou mkoani Zhejiang,China. Eneo hilo limejengwa ndani ya handaki la kujikinga na mashambulizi ya anga, na ni kama “chumba chenye kiyoyozi cha asili” ambapo hali ya joto inadumishwa karibu nyuzijoto 25. Pia kumewekwa chumba cha kusoma vitabu,eneo la kucheza ping-pong, na viti 400 kote katika eneo hilo. Aidha, maji ya kunywa, mtandao wa internet,na dawa za kukabiliana na joto hutolewa bila malipo, hivyo eneo hilo limekuwa la burudani chini ya ardhi lenye huduma kamili, na kuwapatia wakaazi na watalii mahali pazuri pa kukaa wakati wa majira ya joto.
