Mgomo wa wafanyakazi wavuruga safari za anga nchini Kenya

Mgomo wa wafanyakazi wa anga ulioanza jumapili iliyopita nchini Kenya umesababisha shughuli za usafiri kuvurugika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini humo kwa siku ya pili jana Jumatatu, huku maelfu ya wasafiri wakilalamikia kuahirishwa kwa safari zao au nyingine kukwama wasijue tarehe halisi ya safari zao.

Jumapili iliyopita, Mamlaka ya Kusimamia Viwanja vya Ndege nchini Kenya (KAA), iliarifu kwamba inashughulikia suala hilo kupunguza adha kwa abiria, lakini hali hiyo imeenea katika viwanja vyote vya ndege vya umma nchini Kenya, kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa viwanja vye ndege.

JKIA ni uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Maziwa Makuu, ukiwa na wasafiri 13,000 kwa siku, huku watu milioni 8.6 wakisafiri kupitia uwanja huo kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live