Katibu mkuu wa UM ahimiza kurejesha mazungumzo kati ya Russia na Ukraine

Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stéphane Dujarric amesema, katibu mkuu Bw. António Guterres anataka juhudi za kidiplomasia za hivi karibuni ziwezeshe kurejeshwa kwa mazungumzo kati ya Russia na Ukraine.

Kwenye mkutano wa kawaida na wanahabari, Bw. Guterres amefurahia juhudi za kidiplomasia ikiwemo ziara ya mjumbe maalumu wa Marekani huko Moscow na Kiev. Anataka pendekezo jipya linaziwezesha Ukraine na Russia kurejesha mazungumzo na kutandika njia kwa ajili ya kusitisha vita mara moja bila sharti lolote na kufikia amani kamili ya kudumu, yenye usawa na inayolingana na sheria ya kimataifa.

Bw. Dujarric amesema, wakati huohuo Bw. Guterres ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi dhidi ya  miundombinu ya kiraia na watu wa kawaida wa nchi mbili, huku akitoa mwito wa kusitisha mara moja mashambulizi dhidi ya watu wa kawaida na miundombinu ya kiraia na kuzitaka pande mbili kuweka mazingira wezeshi kwa juhudi za kidiplomasia.

NEW YORK, UNITED STATES – 2024/02/07: Secretary-General Spokesperson Stephane Dujarric attends Tor Wennesland, Special Coordinator for the Middle East Peace Process press briefing at UN Headquarters. (Photo by Lev Radin/Pacific Press/LightRocket via Getty Images)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live