Raia wa kigeni nchini Kenya wana siku 90 kuwa na vibali vya kazi

Kenya imewapa raia wa kigeni wanaoendesha biashara ndogo ndogo siku 90 za kuratibu hadhi yao ya uhamiaji, vibali vya kazi na leseni za biashara.

Msemaji wa Ikulu ya Kenya Bw. Hussein Mohammed, amesema kazi hiyo itaratibiwa na balozi za raia wageni, na kuwapa fursa iliyo wazi na iliyopangwa ya kuratibu ukaazi wao na shughuli za biashara.

Taarifa hiyo inafuatia agizo la awali la Rais William Ruto, kwamba biashara ndogo ndogo kama vile uuzaji wa bidhaa nje na rejareja zinapaswa kutengwa kwa ajili ya Wakenya, na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyabiashara wa kigeni, haswa warundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live