Safu za miche ya miti sasa zimesimama kwa mpangilio huko Shabartai Gacha, Chaganmulun Sumu, Bairin Youqi, Jiji la Chifeng, Mongolia ya Ndani, eneo lililoko ukingo wa magharibi wa Eneo la Jangwa la Khorchin.
Eneo hilo, lililoko pembezoni mwa Eneo la Jangwa la Khorchin, limetekeleza miradi ya kudhibiti jangwana kuongeza uoto wa kijani kulingana na mazingira ya hapo. Jitihada hizi zinatumia vyema sifa za ardhi yenye mchanga, kuzingatia kanuni za urejeshaji wa asili, kutumia aina za mimea asilia inayostahimili ukame, na kutumia mbinu za kisayansi kama vile vizuizi vya mchanga vilivyopangwa kwa mtindo wa gridi na upandaji miti kwa mtindo wa mistari.
