
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Alhamisi ilizindua chanjo ya Ebola ya Ervebo chini ya mfumo wa matumizi kwa watu walio hatarini katika jimbo la kaskazini mashariki mwa Tshopo, huku nchi hiyo ikiongeza juhudi za kudhibiti mlipuko unaoendelea wa virusi vya Ebola vya Bundibugyo.
Waziri wa Afya wa DRC Roger Kamba alizindua rasmi chanjo hiyo huko Kisangani, mji mkuu wa Mkoa wa Tshopo, huku wafanyakazi wa huduma ya afya na walio mstari wa mbele wakiwa miongoni mwa makundi ya kwanza kupokea chanjo hiyo.
Kamba amesema wameamua kutumia chanjo ya Ervebo ili kuwalinda kwanza wale walio mstari wa mbele, yaani watoa huduma za afya, lakini pia watu ambao wamekuwa wakiwasiliana na wagonjwa, akieleza kuwa zaidi ya dozi 50,000 za Ervebo zimepokelewa.
Wizara ya Afya ilisema kwenye mtandao wake wa X kwamba uzinduzi huo ulikuwa hatua muhimu katika mwitikio wa Ebola, ikibainisha kuwa chanjo hiyo itaimarisha hatua zilizopo zinazolenga kulinda jamii, kuvunja minyororo ya maambukizi na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.