Tamasha la mawasiliano ya kiutamaduni la Sikukuu ya Mwezi kati ya China na Afrika Kusini 2026 lafanyika Pretoria

Tamasha la mawasiliano ya kiutamaduni la Sikukuu ya Mwezi kati ya China na Afrika Kusini la 2026 lilifunguliwa tarehe 26 huko Pretoria nchini Afrika Kusini, ikiwa ni shughuli muhimu ya kiutamaduni ya kiraia katika “mwaka wa mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika” wa 2026.

Tamasha hilo la siku mbili lina maonyesho ya utamaduni wa Afrika, vyakula vya kichina, maonyesho ya urithi wa kiutamaduni usioshikika na kadhalika. Shughuli za kuonja keki za mwezi, na kujaribu sanaa ya kaligrafia ya kichina zimewavutia watu wengi kushiriki.

Wenyeji walioandaa tamasha hilo wamesema wataweka majukwaa mengi zaidi ya mawasiliano ya kijamii kwa kutumia fursa za sikukuu, na kuendelea kuhimiza mawasiliano ya kiraia kati ya China na Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live