Chuo Kikuu cha Sudan Kusini chazindua kozi ya bure ya lugha ya Kichina

Chuo Kikuu cha Juba nchini Sudan Kusini kimezindua kozi ya bure ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi na wafanyakazi 124 wa vyuo vikuu ili kuimarisha ushirikiano wa kielimu na mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Sudan Kusini.

Ikiandaliwa kwa usaidizi wa Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini, programu hiyo iliyozinduliwa Alhamisi ilivutia wanafunzi 88 na wafanyakazi 36 kutoka Chuo Kikuu cha Juba, Chuo Kikuu cha Upper Nile, na Chuo Kikuu cha Stafford.

Naibu makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Juba anayeshughulikia  masuala ya kitaaluma, Isaac Cleto Rial, aliushukuru ubalozi wa China kwa kuendelea kuunga mkono elimu nchini Sudan Kusini, ikiwemo kutoa fursa za udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa nchi hiyo. Amebainisha kuwa kupata ujuzi wa lugha ya Kichina kunaweza kufungua fursa mpya za kielimu na kitaaluma kwa washiriki. Aliwahimiza kuhudhuria madarasa kwa wakati, kusoma kwa bidii na kujitahidi kupata uhodari wa kitaaluma.

Pia alielezea mipango mingine ya ushirikiano, ikiwemo mechi ya soka iliyofadhiliwa na ubalozi pamoja na msaada kwa wanafunzi wenye ulemavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live