
Kwa mujibu wa wanasayansi, joto kali sana katika milima Alps limesababisha idadi kubwa ya maporomoko ya mawe, baadhi yakipeleka vifo, huku “kwa kiasi kikubwa likisababishwa na msukosuko wa tabianchi”.
Mkurugenzi wa utafiti katika kituo cha taifa cha utafiti wa kisayansi cha Ufaransa (CNRS), Ludovic Ravanel alisema mwaka huu utakuwa mwaka wa rekodi kwa upande wa maporomoko ya mawe na wingi wa mawe yanayotoka milimani karibu kila siku.
Eneo linalozunguka Mont Blanc lililopewa jina la utani “paa la Ulaya” limeathiriwa zaidi. Mwishoni mwa majira ya joto yaliyojaa mawimbi makali ya joto, idadi ya mawe yaliyoporomoka ambayo yamerekodiwa katika Mont Blanc pekee inatarajiwa kufikia 450, Ravanel alisema.