
Mamlaka za Mkoa Unaojiendesha wa Xizang nchini China, zilisema Alhamisi kwamba wakazi walioathirika na maporomoko ya matope katika Kaunti ya Gyirong, wamepewa makazi mapya, na watalii wote waliokwama wamehamishwa.
Jumla ya wanakijiji na wafanyakazi wa ujenzi 499, wote wamepatiwa mahali pa kujisitiri ipasavyo. Wakati huo huo, watalii 555 walioathirika walihamishwa chini ya uratibu wa mamlaka za utamaduni na utalii. Hakuna mtalii aliyekwama.
Wizara ya Rasilimali za Maji ya China Alhamisi ilianza kutoa mwitikio wa dharura wa mafuriko wa ngazi ya IV mkoani humo, huku kizuizi cha ziwa kilichojiunda baada ya maporomoko ya matope kutokea katika bandari ya mpakani ya Gyirong kikikabiliwa na hatari kubwa ya kuvunjika na kupeleka maji ya mafuriko chini ya mto.