Shirika la Kimataifa la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesema, idadi halisi ya vifo kutokana na mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huenda ni kubwa zaidi ya tawimu halisi zilizoripotiwa kutokana na pengo kati ya ufuatiliaji na ugunduzi wa kesi, huku ukosefu wa usalama unaoendelea ukiharibu jitihada za kudhibiti janga hilo.
Shirika hilo limesema, tangu mlipuko huo ulipotokea, zaidi ya kesi 8,000 zimethibitishwa na vifo zaidi ya 4,000 vimeripotiwa, likieleza kuwa, huu ni mlipuko mkubwa na hatari zaidi wa Ebola uliowahi kurekodiwa nchini DRC.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba ongezeko la vurugu mashariki mwa DRC linaendelea kuathiri jitihada za kupambana na Ebola, ikiwa ni baada ya kituo muhimu cha kusafirisha wagonjwa kuharibiwa kwa moto katika kambi ya wakimbizi ya Kigonze mkoani Ituri.
Mlipuko huo uliotangazwa mwezi Mei, sasa umekuwa mlipuko mkubwa wa pili wa Ebola duniani, ukifuatia janga la Afrika Magharibi kati ya 2014-2016.
