Rais wa Botswana asema hatua ya ushuru sifuri ya China yafungua mlango wa fursa kwa Afrika

Rais Duma Boko wa Botswana alifanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Oktoba 12 hadi 17, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini China tangu aingie madarakani. Kwenye mahojiano na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, rais Boko amesema sera ya ushuru sifuri ya China kwa Afrika, imehimiza maendeleo ya kibiashara, kuzidisha uaminifu kati ya Afrika na China, na kuwa nguzo muhimu ya ushirikiano kati ya Kusini na Kusini.

Rais Boko amesema China haijawahi kuwa nchi ya kibeberu, na siku zote inashikilia udhati mkubwa na kuhakikisha kuheshimiana. Amesema China haitajaribu kupata faida zisizofaa kutokana na uhusiano wa pande mbili. Hivyo, hatua ya ushuru sifuri inayotekelezwa na China inasukuma mbele maendeleo ya kibiashara.

Pia amesema, hatua hiyo imefungua mlango wa fursa kwa nchi za Afrika na kupunguza mashinikizo yanayotokana na sintofahamu na mitikisiko katika soko la kimataifa kwa nchi hizo, kuzidisha hali ya kuaminiana kati ya Afrika na China na kuwa nguzo muhimu ya ushirikiano wa Kusini-Kusini. Rais Boko amesema China imetoa mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuendelea kusukuma mbele ushirikiano huo uwe wa kina na wenye ufanisi.

Duma Boko, Botswana’s president, during the United Nations General Assembly (UNGA) in New York, US, on Wednesday, Sept. 23, 2026. The theme of the 81st session of the United Nations General Assembly is “Restoring trust, managing transformation: A United Nations that delivers for all.” Photographer: John Lamparski/Bloomberg

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live