Wanawake wazee wa Kibera nchini Kenya wafurahia soka  

Wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 60 huko Kibera, mjini Nairobi, nchini Kenya, wanakaza nyuzi za viatu vyao na kupiga mpira, wakionyesha kuwa umri si kikwazo cha kuendelea kuwa na shughuli.

Baada ya kazi, timu ya Mugumoini iliyoanzishwa na wanawake hao inakutana uwanjani kufanya mazoezi, kucheka na kuimarisha urafiki wao. Soka inawapa fursa ya kudumisha siha zao, kupumzika na kuendelea kushikamana na jamii yao.

Kwa wanawake hawa, soka si mchezo tu, bali pia ni njia ya kuendelea kuwa na pirika, kuwa na afya njema na kudumisha mahusiano, ikithibitisha kuwa mtu anaweza kucheza bila kujali ana umri wa miaka mingapi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live